Jinsi ya Kujua Simu Original na Fake (Simu Halisi vs Feki)

 




1. Hakiki IMEI Number (IMEI Check)


IMEI (International Mobile Equipment Identity) ni namba ya kipekee inayotambulisha simu yako. Kila simu halisi ina IMEI yake ambayo inaweza kuthibitishwa.


Jinsi ya Kuangalia IMEI ya Simu Yako:

Piga: *#06#

Au nenda: Settings > About Phone > IMEI

Thibitisha IMEI Hiyo:

Tembelea tovuti rasmi ya https://www.imei.info/

Weka IMEI yako — utaona aina ya simu, kampuni, na maelezo yake halisi.

2. Angalia Ubora wa Muundo (Build Quality)

Simu feki mara nyingi hutengenezwa kwa plastiki ya bei nafuu au nyenzo zisizo imara. Zifuatazo ni dalili:

Buttons zinapotikisa au kupinda kirahisi

Logo ya kampuni kuwa tofauti na ile ya asili

Screen resolution kuwa hafifu au  ukungu.

3. Hakiki Mfumo wa Uendeshaji (Operating System)

Simu feki zinaweza kuonyesha kuwa ni Android au iOS, lakini kwa undani haziendeshwi na mifumo hiyo halisi.

Njia ya Kuangalia:

Nenda Settings > About Phone

Angalia toleo la Android au iOS (kama ni ya ajabu au isiyoendana na model, ni feki)

Tumia apps kama CPU-Z au Device Info HW kuthibitisha hardware halisi.


4. Jaribu Kamera na Storage

Simu feki mara nyingi zinakuwa na kamera duni na kumbukumbu bandia.

Piga picha halafu angalia ubora wake.

Nenda Settings > Storage na angalia kama ukubwa unaoonyeshwa ni wa kweli.

Tumia app kama DiskInfo ili kuona ukweli wa storage.

5. Bei Isiyo ya Kawaida

Simu mpya ya bei ya chini kupita kiasi ni ishara ya simu feki.

Mfano: iPhone 14 ikiuzwa kwa Tsh 200,000 = Feki!

6. Nunua Kutoka Kwa Wauzaji Wanaoaminika

Epuka kununua simu kwenye mitandao ya kijamii bila uthibitisho

Nunua kupitia maduka makubwa au online platforms zinazoaminika kama Jumia, Vodacom, au Samsung Tanzania, Tecno Tanzania, Infinix Tanzania N.k 


Hitimisho

Usikubali kudanganywa. Kabla hujanunua simu, tumia hatua hizi kuhakikisha unapata smartphone halisi (original). Angalia IMEI, quality, kamera, na bei. Pia, nunua sehemu rasmi pekee.

Kumbuka:

Smart Tech for Smart People — Rakesh Phones & Tech

Comments

Popular posts from this blog

Vivo X200 FE – The Ultimate Flagship Killer Launching on July 10

🚨 BREAKING: Apple Officially Releases iOS 18.3 – Biggest Update Yet!

Xiaomi 15S Pro Yazinduliwa Rasmi –Simu ya Kisasa Yenye Nguvu na Ubora wa Hali ya Juu